Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amezindua rasmi shughuli za uchimbaji wa madini Vuga Kihitu yaliyopo katika shule ya sekondari ya Bangala na kuwataka wachimbaji kufuata na kuheshimu sheria zilizowekwa ili kulinda na kudumisha amani.

Akimuwakilisha Askofu Dkt. Mbilu katika uzinduzi huo msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju amesema kuwa uchimbaji huo unafanyika kwa mujibu wa sheria za Nchi hivyo kuwataka wachimbaji hao kutokuvunja sheria sambamba na kuwaasa kutambua eneo hilo ni sehemu ya kuwainua kiuchumi.
- Details
SEHEMU YA MATUKIO KATIKA PICHA, Ibada ya kuingizwa kazini kwa msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Mkoani Mara. Mch Eliya Kisarema Bwigeki iliyofanyika tarehe 24/04/2022, Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch Michael Mlondakweli Kanju alimuwakilisha Askofu wa KKKT-DKMs Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu katika Ibada hiyo.

- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa hana mashaka na kazi inayoendelea ya ujenzi wa Kanisa jipya katika Usharika wa Mombo kutokana na kasi na mwenendo mzuri wa ujenzi wa Kanisa hilo.
- Details

“Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka” (Marko 16:6).
Wapendwa katika Bwana, kufufuka kwa Yesu ni tendo la matumaini kwa ajili ya maisha mapya. Wanawake waliokuwa jasiri walipoingia ndani ya kaburi walistaajabu kukuta kaburi tupu, ndipo wakapewa ujumbe huu kuwa msistaajabu Yesu mnayemtafuta amefufuka. Waliondoka kaburini wakiwa na hofu kuu huku wakibeba ujumbe huu wa kufufuka kwa Yesu.

Tendo hili la kufufuka kwa Yesu linadhihirisha maisha mapya ng’ambo ya kaburi. Kwa kufufuka kwa Yesu tunauona ukuu na nguvu ya Mungu ikitudhihirishia kuwa kaburi siyo mwisho wa matumaini yetu.

Dunia tunayoishi imejaa majanga makubwa na hofu nyingi. Katika mwaka huu tunasikia majanga ya vita iliyosababishwa na uvamizi wa Taifa la Urusi kuivamia Ukraine. Vita hivi vimeleta madhara mengi kwa dunia tunayoishi mfano kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa mbalimbali muhimu, vifo kwa watu wasio na hatia kama vile Watoto, Kinamama, wagonjwa mahospitalini, kuharibika kwa miundo mbinu ya muhimu na mengine mengi ya kutisha. Haya yote yanaleta simanzi mioyoni mwa walio wengi.

Lakini ujumbe wa kufufuka kwa Yesu unaamsha maisha mapya na kuleta furaha mpya kuwa hata katikati ya giza nene bado lipo tumaini kuu. Yesu aliyesulibiwa sasa yu hai na anatupa tumaini la uhai kwetu sisi sote tunaomwamini. Kaburi kwetu si kitu cha kutisha tena kwakuwa yeye tunayemwamini ameshinda nguvu za kabaru na kuzimu.

Tuungane na wanawake hawa jasiri kuubeba ujumbe wa kufufuka kwa Yesui ili uwafikie watu wote duniani.

Page 84 of 124

