Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mchungaji Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameisihi Halmashauri ya Mipango na fedha kuketi na kupitia mpango mkakakati wa Dayosisi kwa umakini mkubwa kuchambua na kutoa maoni yenye tija ili utekelezaji wake uweze kuja kuwa na tija.

Askofu Dkt Mbilu ametoa rai hiyo leo tarehe: 22/03/2022 wakati akifungua kikao cha Halmashauri hiyo ya Mipango na fedha ya Dayosisi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Utondolo Wilayani Lushoto.

Halmashauri hiyo inajadili na kupitisha mpango mkakati wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ili upelekwe kwenye Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kuujadili na kuupitisha rasmi mpango mkakati wa Dayosisi na baaadae uweze kutumika katika Dayosisi nzima. Mpango Mkakati huo ni wa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2022 hadi 2026.

Katika ufunguzi Askofu Dkt Mbilu alihubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Injili ya Luka 14:28, na kuongeza kuwa ni imani yake utendaji kazi wao utampa Mungu Utukufu kwani mpango huo utakuwa ni Dira ya Dayosisi.

- Details

TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA MADINI YA DHAHABU – BANGALA
Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, anapenda kuwatangazia wazabuni na makampuni yenye sifa ndani na nje ya Wilaya ya Lushoto kwamba yanakaribishwa kutuma maombi ya zabuni ya kununua madini aina ya Dhahabu katika kata ya Vuga Kijiji cha Kihitu- Bangala (Eneo linalo milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki).Mwombaji aambatanishe kivuli cha leseni hai ya biashara na hati ya usajili ya mlipa kodi (TIN) na aoneshe eneo lake la biashara (Physical Address).Utaratibu wa kutuma maombi, tuma maombi katika bahasha na isioneshe alama yoyote ya utambulisho wa mwombaji. Ada ya maombi ni Tsh. 30,000 itumwe kwenye akaunti namba 41606600224 NED-ELCT MFUKO WA FAIDA.Tuma maombi yako kwa,Katibu Mkuu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,S.L.P 10 Lushoto,Maombi yatumwe kabla ya tarehe 25/03/2022

- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo katika ziara ya kikazi Nchini Poland ambapo anahudhuria mkutano wa kamati ya Ibada na Muziki ya Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF) unaofanyika kwenye mji wa Krakow kwaajili ya kuandaa Mkutano Mkuu utakaofanyika Nchini Poland mwaka 2023.
- Details

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amewashukuru Washarika wa Makorora na kipekee wana Dayosisi kwa ujumla kwa jinsi wanavyoendelea kuuombea uongozi na Dayosisi.
Page 86 of 124

