Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 19/09/2021 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Soni Mtaa wa Kwangwenda, Ibada hii ilikuwa na tukio la Uwekwaji wa jiwe la msingi la kanisa  pamoja na harambee ya ujenzi wa Kanisa la mtaa wa kwang’wenda.

Katika harambee hio Jumla ya  shilingi milioni kumi na moja hamsini na moja elfu na miatano hamsini (11,051,550)  ilipatikana kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo lililowekewa jiwe la msingi.

Harambe hiyo imefanyika  kwenye Ibada ya shukrani iliyotolewa na familia ya Askofu Dkt. Mbilu iliyotanguliwa na zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi wa Kanisa hilo ambalo ujenzi wake ulianza tarehe 8, mwezi Machi mwaka 2012.Katika Ibada hiyo Askofu Dkt. Mbilu aliwashukuru watu wote walio jitoa kwa moyo katika shughuli hiyo.

Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mzee Joseph Jali

Akizungumza muda mfupi kabla ya harambee hiyo Askofu mstaafu Joseph Jali ametolea wito kwa vijana ndani ya Kanisa kujitolea nguvu na vipawa Mungu alivyo wajalia kuijenga Dayosisi kwaajili ya vizazi vijavyo.

Awali akihubiri katika Ibada hiyo Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki , Mch. Michael Kanju ametoa wito kwa wana Dayosisi kuona fahari kulijenga Kanisa la mtaa wa Kwang’endwa kwakuwa ndio mahali  Askofu wao alipozaliwa. 

Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus A. Ketto

Pamoja na hayo yote uongozi wa Kanisa la Mtaa wa kwang'enda  umeomba kiasi cha miti hamsini (50) kwaajili ya shughuli ya kutengeneza thamani za ndani za Kanisa hilo. Kwa kutokana na ombi hilo Askofu Dkt. Mbilu ameahidi kwamba swala hilo litashughulikiwa. Askofu mbilu ameongeza pia   kwa kupitia Halmashauri kuu ya KKKT-DKMs na Idara zinazo husika utaandaliwa utaratibu maalumu ili kufanikisha jambo hilo.

Ujenzi wa Kanisa la mta wa kwang’wenda hadi sasa umegharimu kiasi cha Tsh. milioni 36.48 na hadi kukamilika kwake zinahitajika kiasi cha Tsh. milioni 97.46