Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo ziarani Nchini Ujerumani yenye lengo la kuimarisha urafiki na amepata wasaa wa kutoa taarifa mbalimbali juu ya urafiki na hali ya Dayosisi kwa sasa katika sharika na vituo mbalimbali. Ziara hii ya Baba Askofu Dkt. Mbilu nchini Ujerumani inatoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki wa kihistoria kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na marafiki waliopo nchini humo wenye urafiki na Sharika na Vituo vya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.


"Askofu Mbilu. nimekuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na marafiki zetu na baada ya hapo niliingia kwenye mazungumzo rasmi na kujikita zaidi katika kutafuta namna ya kuimarisha ushirikiano uliopo na mahusiano kati yetu na marafiki zetu waliopo hapa Ujerumani"-Askofu Dkt. Mbilu.

Picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu na viongozi mbalimbali wa vikundi vyenye urafiki na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. kushoto kwa Baba Askofu ni Mkuu wa Jimbo la Vlotho Mch. Dorothea Goudefroy na kulia kwa Baba Askofu ni Mkuu wa Jimbo la Minden Mch. Michael Mertins. Wengine ni wajumbe kutoka sharika na vituo mbalimbali.

KATIKA PICHA,  Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu (WAPILI KUTOKA KULIA) akiwa na  viongozi wa kamati ya Undugu kutoka Hainberg Gymnasium Göttingen wenye Urafiki na Shule ya Sekondari Lwandai  pamoja na shule ya Irente Rainbow School.Shule zote hizi mbili zinamilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.