Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametoa salamu za mwaka mpya wa 2023 kutoka kitabu cha Ayubu 22:21. “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. 

Askofu Dkt. Mbilu akihubiri katika Ibada ya Jumapili na mwaka mpya 2023 leo tarehe 01/01/2023 katika Jimbo la Kusini Usharika wa Vuga ametoa wito kwa washarika na wakristo kwa ujumla kufungua mawazo nakumjua Mungu zaidi katika mwaka huu wa 2023 ili mema yaambatane nao. “Mungu tunaye paswa kumjua zaidi na zaidi uso wake hautatuacha”.

MKUU WA JIMBO LA KUSINI: MCH. ISSAI MWETA

Kwa upande wake, Mkuu wa Jimbo la Kusini Mch. Issai Mweta pamoja na kuwasihi wana KKKT-DKMs kuendelea kuiombea Dayosisi amewakumbusha wakristo wote kuombea amani ya nchi pamoja na kudumisha umoja.