Askofu Mteule Mch. Dkt. Msafiri J. Mbilu yupo ziarani katika Mission ya Kigoma ambapo ameshiriki katika kikao cha maandalizi ya Mission hiyo inayoandaliwa kuwa Dayosisi.

 Askofu Andrew Petrol Gulle na Katibu Mkuu Bw. Rigath Mille wa KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria na Askofu Dkt.Abednego N. Keshomshahara na Katibu Mkuu Mch. Elimerek Kigembe wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Magharibi pia wameshiriki katika kikao hicho.

Wahitimu wa Muziki (Tarumbeta) wakiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wao ndugu Michael Kivulenge wa kwanza kutoka kulia mara baada ya Ibada Kanisa Kuu Lushoto. Leo tarehe 21/02/2021

Picha za matukio mbalimbali ya kuaga  mwili wa aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Prof. Vincent Kihiyo,Katika ukumbi wa mihadhara Sekomu na Nyumbani kwa Marehemu.