Uncategorised
- Details
Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS) imefanya Mkutano Mkuu wa 3 baada ya miaka 125 ya Injili ulioanza tarehe 25-26/11/2020 ikumbukwe mkutano huu ulikuwa na ajenda kuu moja ya Uchaguzi wa Askofu mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na viongozi wengine.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuratibu shughuli za mkutano mkuu wa uchaguzi wa Askofu ni Askofu Mstaafu Dkt. Paulo Akyoo toka KKKT Dayosisi ya Meru ambaye baada ya uchaguzi alimtangaza Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye chaguliwa na Wajumbe wa mkutano Mkuu kuwa Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kupata kura 194 sawa na 89.4% .
- Details

Leo tarehe 06/11/2020 imefanyika Ibada ya mazishi ya Mch. Yesaya M. Zahabu katika Usharika wa Msongolo aliyeitwa mbinguni tarehe 03/11/2020. Mchungaji Yesaya Zahabu alikuwa akihudumu katika Usharika wa Kwalukonge. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA libarikiwe.
Page 123 of 125



