MATUKIO KATIKA PICHA. Mkesha wa Maombi kuiombea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kutoka Jimbo la Tambarare Usharika wa Muheza Tarehe. 26/07/2024

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, umeupongeza uongozi na wafanyakazi wa shamba la Irente Farm kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuongeza juhudi ili shamba hilo linalomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki lizalishe zaidi kulingana na ukubwa wake.

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), limewatoa hofu waumini kuhusu uuzwaji wa mali za kilichokuwa Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU, kinachomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Upendo Media, Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Malasusa na Askofu Dkt. Msafiri Mbilu wa KKKT-DKMs wamesema, Kanisa linaitunza jambo hilo kupitia KKKT-DKMs na kuwataka waumini wa KKKT nchini kote kuwa na utulivu wakati jambo hilo likifanyiwa kazi. "Napenda kuwajulisha waumini wote, uongozi wa KKKT-DKMs umekuwa ukifanyia kazi jambo hilo na ni matumaini yangu kuwa jambo hili litapata muafaka na kupewa taarifa rasmi. " alisema Askofu Dkt. Mbilu. Viongozi hao wametoa taarifa hiyo kufuatia tangazo la mnada wa eneo la Chuo hicho lililoonekana kwenye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii na hivyo kuwaomba waumini kutulia. "Ni kweli tupo kwenye changamoto lakini jambo hili bado halijawa nje ya uwezo wetu na tunaamini kila kitu kitakwenda vizuri," alisema Askofu Dkt. Mbilu.

Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju amesema kuwa kutokana na uwepo wa  mmomonyoko wa maadili katika jamii Kanisa limeona ni vema kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wainjilisti wa Dayosisi ili wakawe chachu na kutatua changamoto hiyo katika jamii.