KATIKA PICHA: Mkuu mpya wa Wilaya ya Lushoto Bw. Zephania Stephan Sumaye  leo tarehe 29/08/2024 ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yaliyopo Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga kwa lengo la kujitambulisha kwa Uongozi wa Dayosisi. Bw. Zephania  Sumaye alipokelewa na watumishi wa Ofisi Kuu ya KKKT-DKMs na kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na  mwenyeji wake Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.