Uncategorised
- Details

KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI
S.L.P. 10 (SIMU 027 – 2660027 / FAX 027 -2660092) LUSHOTO TANGA TANZANIA
E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki inapenda kutangaza nafasi ya kazi kama ilivyoainishwa.
NAFASI: Meneja wa Hoteli (Nafasi moja 1)
Majukumu na wajibu wa Meneja wa kituo ni pamoja na:
- Details

Leo tarehe 05/09/2022 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amefanya ziara rasmi ya kikazi Jijini Dar es Salaam na amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mzee Yusufu Makamba pamoaja na Canal Mstaafu Peter Sameji ambaye ni mjumbe wa Kamati ya wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, waishio Jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hii ni kwa ajili ya maendeleo ya Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI).
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru Washarika wa Usharika wa Shume kwa mambo mengi na mazuri wanayoyafanya ya kuijenda Dayosisi na kipekee mchango mkubwa ambao wanaendelea kuutoa kwaajili ya uchangiaji wa Deni la Dayosisi.
- Details
"Pandeni milimani, Mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana".Hagai 1:8. Leo tarehe 03/09/2022 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza harambee ya ujenzi wa Kanisa katika Usharika wa Kabuku, Jimbo la Tambarare. Askofu Dkt. Msafiri Mbilu alianza harambee hiyo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 200,000/= (LAKI MBILU). Baada ya harambee yote kufanyika kiasi cha Tshs. 17,695,000/= kilipatikana Ikiwa ni fedha taslimu Tshs. 14,695,000/ huku ahadi ikiwa Tshs. 3,000,000/=

Page 71 of 124

