Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 21 Novemba, 2021 ameongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika wa Mgwashwi, Jimbo la Kusini.
Imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mgwashwi ambapo jumla ya vijana wapatao 140 walibarikiwa na wawili kati yao walibatizwa.
Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu amewakumbusha vijana hao walio barikiwa kutokuondoka katika kweli ya neno la Mungu na kamwe wasiyumbishwe na mafundisho potofu ya neno la Mungu yaliyo kisiri katika nyakati hizi.
- Details

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju ameupongeza uongozi wa kituo cha Redio Utume Fm chini ya Kaimu meneja wa kituo hicho Bi. Evelyne Balozi Mariki kwa kuendeleza maono ya Dayosisi ya kueneza Injili kwa wote.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Mawasiliano wa KKKT, ndugu Erick Adolph ambae ametembelea Makao Makuu ya KKKT-DKMs leo tarehe 19 Novemba, 2021.
- Details

Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;Nitakushauri,jicho langu likikutazama.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amewataka viongozi walio pewa dhamana ya kusimamia mali za Dayosisi kuendelea kuwa mawakili wema kwa kufanya kazi kwa uamainifu, uadilifu na uwazi kwakuwa wameaminiwa na yeyeto atakayefanya tofauti lazima ataulizwa.
Page 98 of 124

