Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 12/12/2021 ameongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika wa Kanisa Kuu (Cathedral) Lushoto,ambapo jumla ya vijana 86 wamebarikiwa na watano kati yao walibatizwa.

 

Kulingana na kalenda ya matukio ya Dayosisi Baba Askofu Dkt. Mbilu anahitimisha matukio haya huku jumla ya vijana walio barikiwa ikiwa ni   1888 na Wakristo watu wazima waliobazitwa kwa mwaka huu ni 286.

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akimbatiza mmoja wa vijana walio batizwa 

Baba Askofu amewashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa matendo hayo Mkuu yaliyo tendeka katika kipindi hiki.Baba Askofu ameendelea kusisitiza yeye akiwa  mmoja wa wadhamini wa mali za Dayosisi atahakikisha kwa kushirikiana na viongozi wengine mali za Dayosisi hazichezewi na zinabaki kuwa salama.

Kwa upande mwingine Askofu Dkt. Msafiri Joseph mbilu kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki amemtambulisha Mch. Godfrey Tahona Walalaze kuwa sasa ndiye Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki. Hii nikutokana na kuthibitishwa na Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki aliyo keti hivi kalibuni.Mwingine aliye thibitishwa na Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ni CPA  Peter Singano ambaye sasa rasmi ndiye Mkurugenzi wa Fedha na utawala  KKKT-DKMs

 

Mch. Michael Mlondakweli Kanju,Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs (Kushoto), Mch. Godfrey Tahona Walalaze ,Katibu Mkuu KKKT-DKMs,katika picha na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

Katika Risala ya vijana waliobarikiwa kipekee wamemshukuru Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki.Mzee Mathayo Joseph Jali kwa moyo wake na kuona kwamba Watoto wake, wajukuu na vitukuu vyake vinapata elimu,ameonesha juhudi hizo kutokana na maadhimisho ya miaka 60 ya ndoa yake na Bibi Sara Jali kwamba kipaumbele cha maadhimisho hayo ameamua kuweka alama katika Shule ya  BANGALA Lutheran Junior Seminary inayo milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki.

 Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki.Mzee Mathayo Joseph Jali  pamoja na Bibi Sara Jali

Vijana hao wamewashukuru walimu wao waliowafundisha mafundisho sahihi ya neno la Mungu katika kipindi chote cha miaka miwili,Mch . Edward Msocha,PW Eveline Shekindo , Mwj. Naftari Siafu na Ester Mahimbo.Darasa hilo pia lilikabidhiwa kwa Mch. Anderson Kipande,hadi leo vijana hao wanapo barikiwa darasa hilo limekuwa chini ya Mch.Emmanuel Mweta na Mch. Charles Lumwe.

Mafundisho hayo sahihi waliyo yapata vijana hao yamepelekea kukiri mbele ya Baba Askofu kuwa watakuwa vijana wenye nidhamu, watiifu sasa wanapo ingia katika rika la watu wazima baada ya kubarikiwa kwao na kuongezwa kuwa kamwe hawata yumbishwa na mafundisho potofu ya Neno la Mungu yaliyo ikumbu Dunia katika kipindi hiki.

 

 

 

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akipokea   taarifa ya Tume Maalum ya kupitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Dayosisi kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume hiyo W.S Msagati, taarifa hiyo imekabidhiwa  mbele ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe 10/12/2021.

Baba mzazi wa Askofu wa KKKT - Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Mch. Gehaz Malasusa amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 8, Disemba 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, anawatakia waumini na Watanzania wote kwa ujumla, heri na fanaka katika kuenzi kumbukizi ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.