Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,amewapongeza washarika wa Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Saruji kwa moyo wakujitoa katika kumtumikia Mungu.

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 29/11/2021 kwenye Ibada ya uwekwaji wa jiwe la msingi na ufunguzi wa darasa la Watoto wa shule ya Jumapili, mahali ambapo Watoto hao wataabudia.
- Details

Leo tarehe 28/11/2021 ni siku ya Bwana ya kwanza katika maajilio, advent ya kwanza.kila mwaka wanawake wanapata nafasi ya kuongoza Ibada na kufanya maombi na maombezi kwa ajili ya familia,Sharika,Majimbo na Dayosisi kwa ujumla.Sharika zote za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki zimeungana katika maombi hayo.

Katika Ibada iliyoongozwa na wanawake, Kanisa Kuu Lushoto wametambua umuhimu wa mfuko wa maendeleo na kumuomba Mungu malengo na maono ya viongozi wa Dayosisi yapate kutimia kupitia mfuko huo.


Ibada hiyo iliyo ongozwa na wanawake katika Kanisa Kuu Lushoto imeongozwa na Mwinjilisti Esther Mahimbo, na Mwenyekiti wa wenzi wa wachungaji kutoka KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Janeth Kalinga ndiye aliye hubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Mathayo 24:42-44.

Kwa upande mwingine Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru UEM kwa kuratibisha na kuwezesha warsha iliyo unganisha kundi kubwa na lililokamili la wake wa wachungaji na mashemasi kutoka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani,katika warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano SEKOMU.

Askofu Dkt. Msafiri Mbilu pia amewashukuru wake wa wachungaji kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa kutoa kiasi cha Tsh 500,000 (Mbegu) ili wake wa wachungaji na mashemasi waanzishe kikundi cha Vicoba ambacho, Baba Askofu ameahidi uongozi utasimamia kikundi hicho.


Mbali na kiasi hicho walicho kitoa wameweka alama ya kuimarisha undugu kati ya Dayosisi hizi mbili, katika vituo vya Dayosisi kama ifuatavyo.Shule ya Watoto wenye ulemavu wa akili Irente Tsh. 500,000, Kituo cha mafunzo na malezi bora kwa Watoto yatima Irente Tsh.500,000 pamoja na Tsh 500,000 kwaajili ya Shule ya wasioona Irente.

- Details

Leo tarehe 27/11/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Mshihwi kanda ya Magoma, Jimbo la Tambarare, ambapo vijana wapatao 63 walipata kipaimara.
Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Mshihwi.
Katika risala ya vijana hao waliopata kipaimara wamemshukuru Baba Askofu Dkt. Mbilu kwa kutenga muda wake na kushiriki katika Ibada hiyo, kipekee wameushukuru uongozi wa KKKT-DKMs pamoja na watenda kazi wengine wa KKKT-DKMs kwa namna wanavyo fanya kazi kubwa ya kuirejesha Dayosisi katika hadhi yake ya awali.
Katika siku hii vijana hao wanapothibitisha imani yao ya Kikristo waliyobatizwa nayo walipo kuwa watoto wadogo wameungana na uongozi wa Dayosisi katika kuunga mkono masuala ya elimu kwa kuchangia jumla ya Tsh.189,000.
Awali Baba Askofu aliyeambatana na msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch. Michael Mlondakweli Kanju walipata nafasi ya kufungua nyumba ya mtumishi katika Usharika huo wa Mshihwi kanda ya Magoma.
Page 96 of 124

