Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na Maaskofu wapatao 18 wameshiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na Kusimikwa kazini Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mchungaji Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.Waziri Mkuu ameshiriki Ibada hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

Kati ya Maaskofu hao walio hudhuria Ibada hiyo ya aina yake kutokea katika historia ya KKKT Dayosisi ya KaskazinI Mashariki iliyo nogeshwa na kumbukizi ya Kuzaliwa ya Askofu Mch.Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,

iliyofanyika katika Kanisa Kuu Lushoto (Cathedral)  alikuwepo Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt. Fedrick Shoo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Angikana Tanzania Maimbo Mndolwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Nchini Kenya Johanes Melio.

Mkuu wa KKKT Akihubiri ujumbe wa neno la Mungu kutoka kitabu cha Yoshua 1:9,  alimkumbusha Askofu Joseph Mbilu kuwa ameitwa na Mungu kuhudumia Kanisa lake  hivyo anao wajibu na jukumu la kufuata sheria zake ndipo atakapo fanikiwa katika mambo yote.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameahidi kushughulikia changamoto zote zilizokuwa zikikwamisha  ustawi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU na kumuagiza Mchungaji Askofu Dkt.Msafiri Mbilu kutimiza madai ya kisheria kama ambavyo serikali ilielekeza.

 

Kuhusu madeni yanayo kikabili SEKOMU Waziri Mkuu alisema serikali itaharakisha mchakato wa kupitia maamuzi mbalimbali yaliyochukuliwa kabla na ikiwa kanisa litashughulikia madai hayo ya kisheria, chou kinaweza kuanza udahili wakati madeni yanayo kikabili yakiwekea utaratibu mzuri wa kulipa taratibu.

Awali Mbunge wa Wilaya ya Lushoto Mhe.Shabani Shekilindi na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Yusuph Makamba walimueleza waziri Mkuu umuhimu wa SEKOMU kwa ustawi wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Mkoa wa Tanga  kwa ujumla wake wakimsihi kuingilia kati jitihada zinazo fanywa na Dayosisi ili kukirejesha chou hicho kama awali.  

Akitoa neno la shukurani kwa Mgeni rasmi, Mkuu wa Kanisa Askofu Dkt. Fedrick Shoo alimuomba Waziri Mkuu kuona namna ambavyo Serikali inaweza kuipunguzia kanisa mzigo wa kodi katika vituo vya kanisa hali inayo changia vishidwe kujiendesha, sambamba na hiyo amemsihi pia kupunguza vikwazo kwa wamisionari wanao kuja kujitolea hapa Nchini.

Viongozi wengine wa ngazi mbalimbali walio hudhuria katika ibada hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela

alieambatana na sekretarieti ya Mkoa, wakuu wa Wilaya za Lushoto, Korogwe na Mkinga, Wakurugenzi wa Halmashauri, baadhi ya wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Tanga, viongozi wa vyama vya siasa, wasaidizi wa Maaskofu, wenza wa maaskofu na wachungaji.

Viongozi wengine ni kutoka UEM (United Evangelical Mission), Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT, Kanisa Katholoki Tanzania…