Mahubiri ya Baba Akofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu Leo tarehe 16/05/2021

Ndugu zangu wapendwa katika Bwana. Siku hii ya leo tumeamua iwe siku ya KANTATE DOMINO kutokana na maandalizi yatu ya siku zilizopita. Kimsingi siku hii ni ya kusubiri ahadi ya Baba kutupa Roho Mtakatifu baada ya kupaa kwa Bwana. Lakini tendo lenyewe la uimbaji linaongozwa na huyo Roho wa Mungu pia. Kuimba ni kipawa kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Tunapotafakari juu ya Kantate siku ya leo, tunapewa Neno la Mungu kutoka Zaburi ya 150:1-6 Zaburi ya 150 ndiyo ya mwisho kwenye Kitabu cha Zaburi. Kitabu hiki cha Zaburi kinakusanya nyimbo nyingi, mashangilio na sala vipindi mbalimbali mf. Zaburi ya 23 ni sala. Zaburi yote ya 150 ni ya kumsifu Mungu. Zaburi hii imejaa ujumbe mmoja tu wa kuwahimiza watu wansifu Mungu. Himizo hili la kumsifu Mungu linaanzia katika Zaburi 146.

 

Ukisoma kwa makini utaona kuwa Zaburi hii inatoa mkazo wa mambo matatu:

  1. KILA MAHALI MSIFUNI MUNGU (150:1)
  • Katika patakatifu pake – yaani mkiwemo hekaluni au kanisani.

“Msifuni Mungu katika Patakatifu pake” 

Mahali sahihi na pa kwanza kumsifu Mungu ni katika patakatifu pake.

Mahali patakatifu ni pale ambapo watu wameamua kuketi na kumsifu Mungu. Hata nyumbani panaweza kufaa na kuwa mahali pazuri pa kumsifu Mungu.

 

Wengine wanamsifu Mungu hata wanapokuwa Maofisini kwako

Sokoni, na maeneo mbalimbali ya kazi. Msifuni Mungu katika anga la uweza wake.

Wengine wanamsifu wakiwa Baa wanalewa.

 

  1. SABABU ZA KUMSIFU MUNGU

Kwa matendo yake Makuu mf. Uumbaji wake, utunzani wake kwetu, ukombozi wake.

 

Wana wa Israel walipovuka tu bahari ya Shamu walikaa chini nakuimba.

Kutoka 15:1 “Ndipo Musa na Wana wa Israel wakamwimbia Bwana wimbo huu kusema:

Nitamwimbia BWANA, kwa naana ametukuka sana; Farasi na mpanda Farasi amewatupa baharini…”

Sisi Wakristo tunapaswa kumsifu Mungu kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu.

 

Sisi wana KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki tunapoangalia jinsi Mungu alivyotuvusha katika mengi, tunaona tunayo sababu kubwa ya kumsifu na kumwimbia Mungu.

Hata hapo nyumbani kwako tazama tu unayo sababu ya kumsifu na kumtukuza Mungu kwa kadri ya wingi wa fadhili zake kwako.

  1. TUMSIFU MUNGU KWA NJIA ZOTE MBALIMBALI ALIZOTUJALIA (150:3-5)

Msifuni kwa mvumo wa baragumu

Vyombo vya muziki vyote vitumike kumsifu Mungu na kisibaki chombo chochote kushiriki kumsifu Mungu.

Niliposoma somo hili nimejiuliza Lakini kwanini baragumu kwanza?

Baragumu haitumii Noti maalum – inanguruma tu. Inavuma tu. Imekaa kama pembe.

Nyakati za Wayahudi sauti ya baragumu ilitumika kuita watu kwa matukio mbali mbali, kama kusanyiko la kusoma sheria, kutangaza kutawazwa kwa mfalme wa Kiyahudi na pia kutangaza vita. Na sasa tunasubiri baragumu ya mwisho  Yesu kurudi kulichukua kanisa lake.

 Katika Zaburi hii baragumu inatangulia ikialika vyombo vingine vyote vya muziki kushiriki kumsifu Mungu yaani kinanda, kinubi, matari, kucheza, zeze, filimbi na matoazi.  Maana yake kila alichonacho mtu kimsifu Mungu. 

Ala hizi za muziki zinatajwa kuonyesha kuwa kazi ya kumsifu Mungu ni ya kila mtu, usije ukasema mimi chombo changu hakikuwepo.

Mwimba Zaburi huyu anakaza “kila mwenye pumzi na amsifu Bwana”.

 

Hakuna udhuru.

 

Ndugu zangu wapendwa tunapoalikwa kumsifu na kumwimbia Mungu tunapaswa kutambua haya yote:

  1. Kazi ya kumwimbia na kumsifu Mungu niya wote. Usijitoe. Humu Kanisani kuna wasioimba. Wanatega. Tusitege kuimba.
  • Kukosa vitabu, tunavizia tu.
  • Hatutoi sauti yote
  1. Kila kundi lina namna yake: hata humu ndani wengine magitaa, wengine Key Boards, wengine ngomank. Zote hizizi tumike vizuri kumsifu Mungu.
  2. Tuwe waangalifu tunapocheza: Tuangalie marika (mf. si lazima kucheza kama Rose Mhando)
  3. Utaalamu utumike katika kutunga nyimbo, kutamka maneno

Mf. Wamasai – Yesu ni Mamba…

Mf. Wasambaa “Ntaja Tosheka”

  1. Tuimbe majumbani mwetu ili Watoto wazijue nyimbo zetu
  • Mame nzughuia ni miyo Mima Ee…

 

Mungu atusaidie kila mwenye pumzi amsifu Mungu. Pumzi Mungu aliyokupa uitumie vizuri ili imsifu yeye daima. Pumzi ni mali ya Mungu anayeweza kuondoa kwa wakati wowote ule (corona na magonjwa mengine).

  • Tena wimbo wetu ume mpya huku ukiyatangaza matendo makuu ya Mungu.
  • Tumwimbie popote tulipo katika anga la uweza wake.