Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza nakuwatakia baraka za Mungu katika masomo yao wanafunzi wanaoenda masomoni katika Chuo cha Biblia na Theolojia Mwika pamoja na Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.

Amewakumbusha kuwa wanaenda kuiwakilisha KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na wanatumwa na Dayosisi kwa ujumla hivyo wakajitahidi kusoma kwa bidii sana na kujiepusha na mambo yasiyofaa, kusimamia yale ambayo niya Kanisa ili mwisho wa siku wafaulu vizuri na kuja kuitumikia Dayosisi.

Askofu Dkt. Mbilu ameagana na wanafuzi hao leo tarehe 20/10/2021 kwenye Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Kwa kozi ya Theologia katika Chuo cha Biblia na Theolojia Mwika   wanafunzi wanaoenda kusoma wapo watano ambao ni Yona Simoni Mgonja, Ester Godwin Kivuma, Eliwine Jackson Mdundwa, Mambazi S. Mgonda pamoja na Janeth Yacob Doop.

Wanafunzi wawili Jerry Godfrey Mdoe pamoja na Peter Steven Shekikwa wao wanaenda kusoma  kozi ya Shahada yaani Bachelor of Divinity katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwa mwaka wa masomo 2021/2022.