Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza washarika wa Usharika wa Mkata Mtaa wa Magamba kwa kazi kubwa na nzuri ya ujenzi wa Kanisa unaoendelea.


Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 22/10/2021, alipokuwa anaongoza Ibada ya uwekwaji wa Jiwe la Msingi, Katika Usharika wa Mkata Mtaa wa Magamba.


Mtaa huo wa Magamba ulianzishwa mwaka 2012 ukiwa na waumini saba na sasa unajumla ya waumini 54.