Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi wakati alipokuwa akihesabiwa na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi  ndugu Lazaro Henry Mnyawamikatika makazi yake Chatllon Lushoto Tanga leo Tarehe 23 Agosti, 2022 ambapo zoezi hilo lilimhusisha yeye mwenyewe, mke wake, vijana wake pamoja na watu wote waliolala kwenye makazi hayo.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu mara baada ya kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ameendelea kutoa wito kwa wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi

Askofu Dkt. Mbilu ametoa wito huo leo tarehe 23/08/2022 na kuongeza kuwa maswali yanayo ulizwa katika zoezi hilo ni maswali rahisi hivyo kuwasihi watu wote kutokuwa na hofu yoyote na kujibu maswali  wanayouliza kwa usahihi kwa maslahi mapana  ya taifa.

Sensa imeanza kufanyika leo na inatarajiwa kuendelea kwa siku sita, ili kutoa fursa kwa Watanzania wote kuhesabiwa. Hii ni sensa ya sita kufanyika baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, ambapo nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.