Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imepata kibali cha ajira 6 za Watumishi wa Kada za afya kwa ajili ya Hospitali na vituo vya afya.

Sifa za waombaji ni kama ifuatavyo;

  1. DAKTARI DARAJA LA II (NAFASI 1)

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo vikuu/ Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika)

  1. AFISA MUUGUZI DARAJA LA II (NAFASI 1)

Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurses and Midwifery Council).

  1. TABIBU DARAJA LA II (NAFASI 1)

Waombaji wawe na Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  1. OCCUPATIONAL THERAPIST II (NAFASI 1).

Kuajiriwa wahitimu wenye Stashahada Mtoa tiba kwa Vitendo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  1. MUUGUZI DARAJA LA II (NAFASI 1).

Waombaji wawe na cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na Kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).

  1. MTEKNOLOJIA WA DAWA MSAIDIZI (NAFASI 1)

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa (Certificate in Pharmaceutical Technology) kwa muda wa miaka mitatu kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council)

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI.

  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe na umri usiopunguza miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato Cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika.
  1. Asiwe mwajiriwa wa serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwana serikali.
  2. Mwombaji aliyewahi kuajiriwa serikali na kupata cheki namba, atatakiwa kuzingatia utaratibu wa kuomba kibali cha kurejea katika utumishi wa umma na kuendelea kutumia cheki namba baada ya kuach akazi kama ilivyobainishwa kwenye waraka na. CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti 2012.
  3. Mwombaji awe na sifa na weledi kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya kama zilivyoainishwa hapo juu.
  • Waombaji wenye elemavu watapewa kipaumbele katika ajira hii kwa kuzingatia sheria ya watu wenye ulemavu Na. 1 ya mwaka 2010.

 MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA,

  1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  2. Nakala ya cheti cha kidato cha nne au/ na cha sifa au stashahada kulingana na kada ya mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje ya nchi waambatanishe cheti cha ithibati kutoka baraza la mitihani Tanzania (NECTA).
  • Nakala ya vyeti vya Taaluma na Transcript, Aidha waliosoma vyuo vya nje ya nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
  1. Wasifu (CV).
  2. Nakala ya cheti cha Usajili na Leseni hai ya taaluma husika (Full Registration & Valid Licence).
  3. Nakala ya cheti cha Mafunzo kwa vitendo (Internship).
  • Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
  • Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA/ Namba ya NIDA).
  1. Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako Pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa viapo na kusajiliwa na Msajili wa hati, wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.

Maombi yote yatumwe ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 05/09/2022).

Maombi yote yatumwe kwa Ofisi ya Katibu Mkuu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

S.L.P 10 LUSHOTO

Email:  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.