KATIKA PICHA: Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wilayani Lushoto uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Tebweta Mgumba leo tarehe 29/08/2022. Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alishiriki katika ufunguzi huo.Tawi hilo la Bank ya CRDB lipo katika jengo linalomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. OMARY TEBWETA MGUMBA akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Tawi la CRDB Lushoto.Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, akitoa salamu za Dayosisi na kufungua kwa maombi shughuli za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Lushoto.

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO MHE, KALISTI LAZARO, Akizungumza kwenye uzinduzi wa Benki ya CRDB Tawi la Lushoto ambapo ameushukuru Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuruhusu uwekezaji uliowekwa na Benki hiyo katika jengo linalomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

 

Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (ALIYE KUNJA MIKONO) MCH. GODFREY TAHONA WALALAZE

..................................................

Baadhi ya maafisa wa Benki ya CRDB Tawi la Lushoto