Leo tarehe 05/09/2022 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amefanya ziara rasmi ya kikazi Jijini Dar es Salaam na amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mzee Yusufu Makamba pamoaja na Canal Mstaafu Peter Sameji ambaye ni mjumbe wa Kamati ya wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, waishio Jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hii ni kwa ajili ya maendeleo ya Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI).

Katika picha ni Askofu Dkt. Msafiri J. Mbilu,Mzee Yusufu Makamba (Wa pili kutoka kulia) na Canal Mstaafu Peter Sameji (wa kwanza kushoto)

Chuo hiki cha KOTETI kina usajili wa NACTE kwa Namba. KOTETI/HAS/249 kwa sasa kinaenelea kupokea wanafunzi na wale wanao hitaji kujiunga na kozi ya ORDINARY DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCES  – KWA MIAKA 3 wanaendelea kukaribishwa kutuma maombi yao. Sifa za kujiunga ni angalau alama D nne (4) ikiwemo masoma ya Biology na Chemistry na masomo mengine yoyote mawili (isipokuwa masomo ya Dini).