KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI

S.L.P. 10 (SIMU 027 – 2660027 / FAX 027 -2660092) LUSHOTO TANGA TANZANIA

E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki   inapenda kutangaza nafasi ya kazi kama ilivyoainishwa.

NAFASI: Meneja wa Hoteli  (Nafasi moja 1)

Majukumu na wajibu wa Meneja wa kituo ni pamoja na:

  • Kuajiri  kufuatilia utendaji wa wafanyakazi.
  • Kupanga shughuli na kuwapa majukumu wafanyakazi ili kuhakikisha au kuleta tija.
  • Kutengeneza na kusimamia bajeti za uendeshaji wa kituo.
  • Kufanya tathimini za kawaida za uboreshaji wa huduma kwa wateja.
  • Kukusanya malipo na kudumisha kumbukumbu za bajeti, fedha na gharama.
  • Kuunda na kutumia mpango mkakati wa uuzaji wa bidhaa ili kukuza huduma za Hoteli kwa wateja.
  • Kuratibu mawasiliano na vyama, mashirika pamoja na wauzaji wa bidhaa, mashirika ya safari nje na ndani ya Nchi na wapangaji wa mikutano mbalimbali
  • Kufanya tathmini ya utendaji wa hoteli na kuandaa ripoti kila baada ya ya miezi mitatu, sita, tisa na mwaka.
  • Kushughulikia malalamiko na maswali ya wateja ili kukuza biashara.
  • Kusimamia ufuatiliaji wa taratibu za kisheria za Nchi,afya, Usalama, Mapato na Leseni.

Sifa za mwombaji.

  • Mwombaji awe na Shahada ya Ukarimu, Utawala wa Biashara au uwanja unaofaa.
  • Kiwango cha chini cha uzoefu wa mwombaji ni miaka 3 'katika usimamizi wa Hoteli au jukumu kama hilo.
  • Mwombaji awe na uelewa mkubwa wa mambo ya usimamizi bora wa Hoteli pamoja na ujuzi wa programu za kompyuta za uingizaji data.
  • Mwombaji awe na uwezo wa mawasiliano ya kutumia mitandao kama email, facebook, instagram, twiter booking .com, trip advisor na mengine.
  • Mwombaji awe na mawasiliano bora na watu awe na ujuzi wa huduma kwa wateja.
  • Awe na uwezo wa kipekee wa uongozi kwa umakini mkubwa.

Waombaji wenye sifa tajwa hapo juu wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia anuani ifuatayo.

KATIBU MKUU

KKKT-DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI

S.L.P 10,LUSHOTO TANGA.

Ama kwa Email.  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. or This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30th September 2022