MATUKIO KATIKA PICHA: Askofu wa KKKT -Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, Tarehe 25/11/2023 akiwa katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Mtonga aliongoza Ibada iliyokuwa na tendo la kuwabariki Vijana wa Kipaimara,Ibada hiyo ilitanguliwa na ufunguzi wa nyumba ya mtumishi.

Jumla ya Vijana wapatao 171 walibarikiwa na 5 kati yao walibatizwa, Vijana waliobarikiwa  walitoa kiasi cha Tsh 171,000 kwaajili ya kuchangia ulipaji wa deni la Dayosisi, ambapo pia waliomba kuungwa mkono na wazazi,walezi pamoja na washarika walioshiriki katika Ibada hiyo na kufanikiwa kukusanya jumla ya Ths. 2,028,000/= ambapo fedha hizo zimeelekezwa katika kulipa deni la Dayosisi.

MUONEKANA WA NYUMBA YA MTUMISHI USHARIKA WA MTONGA.