Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akikabidhi vyeti kwa Vijana  11 wa KKKT-Dayosis ya Kaskazini Mashariki waliokuwa ziarani nchini ujerumani ambao pamoja na mambo mengine walifika nchini humo kwa ajili ya mafunzo ya  Water project titled water and Sanitation. Askofu Dkt. Mbilu, amegawa vyeti hivyo  katika Ibada ya Jumapili ya tarehe 12/05/2024 iliyofanyika katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Korogwe.

Sehemu ya Vijana hawa amejumuisha Vijana kutoka Usharika wa Mtae ambao una urafiki na Usharika wa St. Marien Gemeinde ilioko katika Mji wa Minden, Ujerumani.

 Walipata nafasi ya kutembelea Sites/viwanda vingi vinavyohifadhia maji taka na kuyabadilisha kuwa maji masafi. Mmmoja wa Vijana hao Jackson Mbilu alieleza kuwa “Maji yote ya mji wa Minden yanakusanywa sehemu moja halafu kwenye hicho kiwanda ndio wanapobadilisha maji hayo kwakutumia vichujo vya aina nyingi na pia kwakutumia Bacteria’s maalum wanawaweka kwenye maji ili kuuwa na kuyasafisha maji.

Tulitembelea Laboratories mbalimbali na kufundishwa na kuelezewa mambo mbalimbali kuhusu maji na kuonyeshwa Water Pumps na namna ya kuyapima maji na kuyajuwa ubora wake kwa matumizi. Tuliombwa tubebe maji kutoka vyanzo mbali mbali wanavyotumia huko katika vijiji nilivyotaja hapo juu na kuvipeleka ili tukifika kwenye hio labaratory yapimwe na maji yalionekana kuwa masafi na mazuri.

Tulihudhuria pia Seminars mbalimbali na kujadili kuhusu maji na namna bora ya kuyatunza na kushauriana kuwa ni nini tunaweza kufanya ili kusaidia vijiji vyetu hususani huko Mtae, Mponde, Moria, Langata N’doye na Mambo.

Tuliendelea kuwa na Majadiliano mengi pale Usharika wa St. Marien Gemeinde na kuzungumzia na Kujadili kuhusu hali ya Water System na pipes walizoziweka Mtae kuwa zinaendeleaje na ziko katika hali gani na kama ni marekebisho yanahitajika yafanyike wapi na lini.

Jackson aliongeza kwa kusema kuwa,katika siku za mwisho ya ziara yetu tuli pewa nafasi ya kutembelea Mji wa Wittenberg ambapo ni Mji alioishi Martin Luther na Kutembelea Kaburi Lake lililopo katika Castle Church at Wittenberg alipozikwa tarehe 22 February 1546 na kutembelea Museum ambapo kumehifadhiwa vitu vingi ikiwemo Joho Lake alilokuwa akivaa na Biblia yake alioitafsiri.

Baada ya hapo tulielekea katika Mji mkuu wa Germany - Berlin na kutembelea Bunge la Ujerumani (Deutsche Bundestag) na pia kutembelea Ukuta/ Gate maarufu la Germany (Brandenburg Gate) Na tuli tembelea Museums mbalimbali na kutembelea na kuona Jengo la Ofisi ya Chancellor of Germany (ni kama Ikulu ya President of Germany) na baadae mwishoni tukawa na Boat trip around the city of Berlin na kuona historical sights nyingi. ALISEMA JACKSON MBILU.

 

Msafara huu uliongozwa na  Raphael Jackson Mrisho  ukijumuisha vijana wengine Neema Ibahati Masanyika  Sifaeli Peter Kibiriti  Mariane Thomas Kibada Christa Abisai Kamwedi , Jeremia Vilhemu Makange , Martine Mbaraka Shau ,Timilai Apelesi Kanju ,Stephen Hokelai,Shelukindo ,Petro Yonas Kadio ,Jackson Msafiri Mbilu.