Ufunuo 14:13“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Madiga kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, anasikitika kutangaza kifo cha Bitrice David Mmbali kilichotokea tarehe 27/05/2024 katika Hospitali ya Mloganzila iliyopo Jijini Dar Es Saalam alipokuwa anapatiwa matibabu.
Marehemu Bitrice Mmbali ni Mtoto wa Mtheologia David Martin Mmbali anayetumika, KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki la Jimbo la Magharibi, Misioni ya Kwamsisi.
Ibada ya Mazishi itafanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 30/05/2024 katika Usharikwa wa Bumbuli na mwili wake utapumzishwa katika makaburi ya Usharika wa Bumbuli.
Uongozi unatoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kipekee Uongozi na wanafunzi wa Shule ya Kisaza high School-Mkata.
BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.