Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Mbilu, alipata fursa ya kupokea ugeni wa kiongozi wa undugu Helga Walter kutoka Hainberg-Gymnasium Göttingen  nchini Ujerumani. 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki tarehe 05/02/2026  , pande zote mbili zilijadili kwa kina namna ya kuendelea kuimarisha na kuboresha undugu uliopo kati yao, hususani katika nyanja za elimu na huduma za kijamii.

Aidha, Askofu Dkt. Mbilu alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa Helga pamoja na wadau wengine wa maendeleo kutoka Hainberg-Gymnasium Göttingen kwa michango yao ya kimaendeleo, hususani katika Shule ya Sekondari Lwandai pamoja na vituo vya diakonia vilivyopo Irente vinavyomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Ziara hiyo ilionesha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano wenye tija kwa manufaa ya jamii.