Tarehe 28/11/2024 Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki walipata nafasi ya kutembelea kituo cha Malezi bora ya Watoto Irente (Irente Children's Home) pamoja na Shule ya Watoto wasioona (Irente School for the Blind) ambapo walipata nafasi yakuona miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ukarabati wa Majengo pamoja na ujenzi wa Green House.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amepiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha kupigia kura cha UWALU kilichopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga tarehe 27 Novemba, 2024.

HABARI KWA UFUPI

Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Malasusa amewataka Wakurugenzi wa Taasisi za Kanisa kuwa wabunifu katika kuendesha Taasisi hizo pamoja na kujifunza kwa wengine ili kuongeza ufanisi na kuweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora kwenye jamii.