Uncategorised
- Details
HABARI PICHA: Picha za matukio mbalimbali ya uzinduzi wa Ushirika wa Wanafunzi wa Kikristo wa Vyuo vikuu na vya kati (USCF) uliofanyika leo tarehe 14/05/2023 katika ukumbi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga.Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye pia ni Katibu wa CCT Mkoa wa Tanga alimumuingiza kazini Mch. Rogers Chamani wa Kanisa Anglican kuwa Mratibu wa USCF Mkoa wa Tanga.

- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewakumbusha Washarika wa Usharika wa Kana na Wakristo kwa ujumla, kuendelea kuomba neema ya Mungu iwaongoze katika kuomba kwa usahihi kama Kristo Yesu alivyo wafundisha wanafunzi wake katika Sala ya Bwana.
Askofu Dkt. Mbilu ametoa wito huo leo tarehe 14/05/2023 wakati akihubiri katika Ibada ya Jumapili ya tano baada ya Pasaka (Rogate) iliyofanyika katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kana, ambapo amesema kwa sasa kumekuwa na uwepo wa walimu wanaofundisha mafundisho potofu yanayo wafanya Wakristo kushindwa kuomba kwa usahihi.
- Details

KATIKA PICHA ni Ujumbe kutoka Tanzania uliohudhuria Mkutano wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani. Katikati ni Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa LWF Mch. Dkt.. Anne Burghadt akifuatiwa na Rais wa LWF Archibishop Musa Panti Filibus.
- Details

Mei 9 mwaka 2021 ilikuwa ni siku iliyotawaliwa na nderemo, vifijo na shamrashamra katika viunga vya Lushoto, siri nyuma ya furaha hii si nyingine bali ni historia mpya kuandikwa, wakristo wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki walipata Askofu mpya, kiongozi ambae atayabeba maono na dira ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki huyu sio mwingine bali ni Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.Mhadhiri huyo mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Silliman cha nchini Ufilipino, aliingizwa kazini katika Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto tarehe 09/05/2021 na kisha yeye kumuingiza kazini msaidizi wake, Mch. Michael Mlondakweli Kanju.
Page 53 of 124

