PICHA ZA MATUKIO mbalimbali ya Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Moses Gao Karata, yaliyofanyika leo tarehe 13/06/2023 katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Mtonga, Ibada imeongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Kanju akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Mch Frank Mtangi.

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Madiga kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mzee Moses Gao Karata kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 10/06/2023 katika Hospitali ya Ocean Road-Dar Es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.
 
Hitimisho ya ziara ya ugeni kutoka Vyuo Vikuu vitano vilivyomuwakilisha Profesa Dkt. Ulrike Ludtke aliyewahi kuwa  mhadhiri wa kilichokuwa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU) mwaka 2008, ametembelea Dayosisi kwa makubaliano kati ya KKKT-DKMs na  chama Cha kiinjili Cha Kimisioni (UEM: United Evangelical Mission) kwa lengo la kuanzisha kozi ya Lugha na mawasiliano (Speech and language therapy).

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni maalum kutoka Vyuo vikuu vitano ambavyo ni, Muhimbili (MUHAS), KCMC/KCMU,Chuo cha Kenyata kilichopo Kenya,Chuo cha Protoria cha Africa ya Kusini na Chuo kikuu cha Leibniz kilichopo Hannover Ujerumani, uliokuja kwa lengo la kutembelea vituo mbalimbali vinavyomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kuanzisha umoja wa Vyuo hivyo na Taasisi ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kwa madhumuni ya kuanzisha kozi ya lugha na mawasiliano ( Speech and language therapy).