Msaidizi wa Askofu wa KKKT-DKMs Mch Michael Kanju (Kushoto) akimakabidhi Mkuu wa Chuo cha Biblia Vuga Mch. Benson Kimweri Kivuli cha kadi ya Pikipiki

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amekabidhi pikipiki 1 kwa Mkuu wa Chuo cha Biblia Vuga Mch. Benson Solomon Kimweri, ikiwa ni hatua za awali za kutatua changamoto ya usafiri  Chuo hapo huku akiagiza pikipiki hiyo kwenda kutumika kwa malengo mahsusi yaliyokusudiwa,

Mzaidizi huyo wa  Askofu Mch. Michael Kanju amekabidhi pikipiki hiyo kwa niaba ya Baba Askofu Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 04/07/2023 katika Makao Makuu ya KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto Tanga.

Hii ni kufuatia ahadi ya Askofu Dkt. Msafiri Mbilu  aliyoitoa mnamo tarehe 28/06/2023  akiwa katika ziara yake ya kikazi kutoa pikipiki kwa ajili ya Chuo hicho cha Biblia Vuga ambapo pia aliueleza uongozi wa Chuo hicho kuwa mipango ya  upatikanaji wa gari kwaajili ya  Chuo hicho bado inaendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Mch. Benson   Kimweri  ameushukuru uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kuwapatia pikipiki hiyo itakayokuwa msaada katika mambo ya usafiri.

Katika kuungana kwa pamoja kuchangia DENI linaloikabili KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kunusuru mali zake zisipigwe mnada sasa unaweza kutumia namba hizi za simu kutoka mitandao ya Airtel Vodacom na Tigo kutuma mchango wako.