Uncategorised
- Details
MATUKIO KATIKA PICHA:- Ibada ya maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Arusha tarehe 21/08/2023.

- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametoa wito kwa wafanyabiashara, wadau mbalimbali wa elimu na maendeleo pamoja na Watanzania kwa ujumla kuungana na KKKT-DKMs kwenye harambee kubwa yenye lengo la kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya Diakonia vya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki itakayofanyika tarehe 18/08/2023 Jijini Dar Es Salaam.
- Details

Jumapili ya leo tarehe 16/07/2023 imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa familia ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye akiambatana na familia yake, wamemtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa namna Mungu alivyomtetea Binti yao Sarah hasa wakati wa Ugonjwa wa CORONA.

Katika Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto,ikiongozwa na Baba Askofu Jacob Ole Moreto Paulo Mameo wa KKKT-Dayosisi ya Morogoro. Askofu Dkt. Mbilu amesema kuwa yeye na familia yake wanawiwa kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyomlinda Binti yao Sarah katika kipindi chake cha Masomo cha miaka 6 nchini China. "Lililokubwa kwetu kama Familia ni kuona jinsi Mungu alivyomtetea Binti yetu hasa wakati wa Ugonjwa mbaya wa CORONA ambao ulianzia pale Wuhan kwenye Chuo ambacho alikuwa anasoma binti yetu.
Wakati wa CORONA tulijaribu kumuondoa Sarah arudi nyumbani lakini tulishindwa kabisa. Pale tuliposhindwa tulinyoosha mikono na kumuachia Mungu, leo mioyo yetu imejaa furaha kubwa tunapoona Sarah amemaliza masomo yake ya Shahada ya kwanza ya Utabibu (Bachelor of Medicine) na kurejea nyumbani salama. Katika furaha hii tumeona tumtolee Mungu Shukrani ya pekee" Amesema Askofu Dkt. Mbilu.

Sadaka iliyopatikana katika Ibada hiyo ya Shukrani ilikuwa fedha taslim Milioni nne na elfu sita (Tsh. 4,006,000), ahadi Milioni tatu na laki nane (Tsh. 3,800,000/=) na kufanya jumla kuu kuwa shilingi Milioni Saba laki nane na elfu sita (7,806,000). Kiaisi hiki kilicho patikana kimeelekezwa kulipia deni kubwa la Dayosisi.Askofu Dkt. Msafiri Mbilu amewashukuru ndugu jamaa na marafiki waliofanikisha kupatika kwa kiasi hicho kitakacho saidia katika ulipaji wa Deni la Dayosisi.

- Details

Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Mhandisi Robert Kitundu amewataka Wakristo wa KKKT kuendelea kuliombea Kanisa na kulisogeza mikononi mwa Mungu ili liendelee kudumu katika Umoja na upendo wa kweli.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo tarehe 09/07/2023 kwenye Ibada ya Jumapili iliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Magharibi Usharika wa Kimara ambapo pamoja na kuliombea Kanisa amewasihi Wakristo kutunza Ulutheri katika kumtukuza Mungu.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt.Msafiri Joseph Mbilu ambaye yupo katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi anayoifanya KKKT-DMP ni mmoja wa walio shiriki katika Ibada hii.

Mchana wa leo Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu atakuwa na mkutano na Wakristo wote wanaotokea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto, Tanga pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo waishio Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 Alasiri. Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano KKKT - Mbezi Beach.

Page 48 of 124

