Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania Dkt. Fredrick Shoo amewataka waumini kujiepusha na  mafundisho potofu ya neno la Mungu ambayo yamejitokeza hivi sasa ulimwenguni yenye kuyumbisha imani za waumini walio wengi.

Askofu Dkt. Shoo ameyasema hayo leo tarehe 28/07/2022 katika mwendelezo wa ziara yake anayoifanya ndani ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuzungukia sharika mama,vituo mbalimba pamoja na kufungua na kuweka mawe ya msingi.Aidha amewataka waumini  kutimilika katika Kristo ili kuweza kujiepusha na mafundisho hayo potofu .

Askofu Dkt. Fredrick Shoo akipanda mti akiwa katika Chuo cha Afya na Sayansi na Shirikishi Bumbuli

Sambamba na hayo Askofu Dkt. Shoo amechangia kiasi cha shilingi laki tano 500,000 kwaajili ya ujenzi wa Kanisa jipya linalojengwa katika Usaharika huo wa Bumbuli huku akitoa wito wa kutunzwa kwa Makanisa ya zamani yaliyojengwa na Wamisionari ili kuwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ametoa shukrani kwa Askofu Dkt. Shoo kwa kuendelea kusisitiza kuhusu umoja katika Kanisa na ushirikiano ili kuendelea kuitenda kazi ya Bwana.

 

Katika Mwendelezo wa ziara yake Askofu Dkt. Shoo ametembelea Usharika wa Bumbuli, Chuo cha Utabibu Bumbuli  pamoja na Hospitali ya Bumbuli,Usharika wa Lutindi na Hospitali ya wagonjwa waakili (Lutindi Mental Hospitali),ambapo viongozi mbalimbali wa dini na Serikali wamehudhuria katika ziara hiyo huku akitazamiwa kuendelea na ziara yake hapo kesho katika Jimbo la Tambarare.

 

Awali Askofu Dkt. Fredrick Shoo alishiriki kwenye Ibada ya asubuhi iliyofanyika Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo alipata wasaa wa kuwasalimu wafanya kazi wa Ofisi kuu ya KKKT-DKMs.

Mapokezi Usharika wa Lutindi

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 27/7/2022 ameanza ziara rasmi ya kuitembelea KKKT–Dayosisi ya Kaskazini Mashariki itakayoambatana na kufungua na kuweka mawe ya msingi na kuongea na wana Dayosisi katika maeneo mbalimbali.


Akiwasili katika eneo la Bwiko Usharika Mteule wa Mkumbara Askofu Dkt. Shoo amepokelewa na mwenyeji wake Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na wana Dayosisi na baadae aliwasili katika Usharika wa Mombo ambapo ameweka jiwe la msingi la Kanisa jipya na kuongoza Ibada ya Shukrani.


Akihubiri neno la Mungu katika Ibada hiyo kutoka kitabu cha Injili ya Mathayo 7:1-5 Mkuu wa Kanisa amekemea tabia za baadhi ya Wakristo kujihesabia haki na kuhukumu wengine hatua inayofifisha vipawa na karama za wengi katika kulijenga Kanisa la Mungu.


Mkuu wa Kanisa amesema kwakuwa hakuna mtu aliyekamilika kabisa hivyo waliowakristo waonyane kwa upendo bila kunyosheana vidole madhaifu ya wengine.


Mbali na hayo Mkuu wa Kanisa ameendesha harambee kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa la Usharika huo wa Mombo na kuchangia kiasi cha shilingi 1,000,000.


Nae Askofu wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Mbilu amewapongeza wanadayosisi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mkuu wa KKKT na kuwasihi kuendelea kujitokeza katika maeneo yote ya Majimbo ambapo Mkuu wa Kanisa atatembelea.


Kesho tarehe 28/07/2022 msafara wa Mkuu wa KKKT utaelekea Bumbuli, ambapo Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo ataendelea na ziara yake katika Jimbo la Kusini kwa kutembelea Usharika wa Bumbuli, Hospitali ya Bumbuli, Chuo cha Utabibu Bumbuli (BUCOHAs) na kisha ataelekea Lutindi ambapo atapata wasaa wa kuwasalimu Washarika wa Lutindi na kutembelea Hospitali ya wagonjwa wa akili Lutindi (Lutindi Mental Hospital).

 

 

MATUKIO KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili iliyokuwa na matukio mbalimbali ikiwemo Ufunguzi wa nyumba ya mwinjilisti pamoja na Ibada ya kipaimara katika Usharika wa Mbaramo ambapo vijana wapatao 85 wamebarikiwa huku mmoja kati yao akibatizwa.Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ndiye aliyeongoza Ibada hiyo.

 

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa elimu kwa vijana juu ya uandaaji na usimamizi wa miradi ni vema sasa ikatolewa katika Dayosisi nzima ili kuwa na vijana wenye uelewa wa kuandaa miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi na kuisaidia jamii.

Askofu Dkt.Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 23/07/2022 akiwa katika Usharika wa Muheza kwenye kilele cha mafunzo ya  muda mfupi ya uandaaji wa miradi,Tathimini Shirikishi ya Mafunzo (Participatory Learning Appraisal) pamoja na Upangaji wa mradi wenye muelekeo wa matokeo (Result Oriented Project ) yaliyoanza tarehe 11/07/2022 hadi tarehe 23/07/2022 yakijumuisha  vijana wapatao 16  wa Usharika huo.

Nimefurahi kwa Usharika,Washarika,Kamati ya miradi  kuwawezesha vijana hawa kupata mafunzo haya hasa kwenda vijijini kuona matatizo yalipo katika jamii kuandika miradi kwa wafadhili itakayo wapatia fedha zitakazo isaidia jamii, HILI NI JAMBO ZURI NALA KUPONGEZA. Alisema Askofu Mbilu.

Awali katika Ibada ya Jumuiya iliyo jumuisha jumuiya zote za Usharika huo iliyo ongozwa na Baba Askofu Dkt, Mbilu katika Usharika huo, amemshukuru Mkuu wa Jimbo la Tambarare Mch. Frank Mtangi, Mchungaji wa Usharika wa Muheza Mch. John Ndimbo wakufunzi pamoja na kamati mbalimbali zilizowezesha kufanikisha mafunzo hayo kwa vijana na kutoa wito kwa Majimbo na Sharika zingine kuiga jambo hilo.