Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru Washarika wa Usharika wa Kange Mtaa wa Maweni kwa namna wanavyo jitoa katika kazi za umoja.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imepata kibali cha ajira 6 za Watumishi wa Kada za afya kwa ajili ya Hospitali na vituo vya afya.

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi wakati alipokuwa akihesabiwa na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi  ndugu Lazaro Henry Mnyawamikatika makazi yake Chatllon Lushoto Tanga leo Tarehe 23 Agosti, 2022 ambapo zoezi hilo lilimhusisha yeye mwenyewe, mke wake, vijana wake pamoja na watu wote waliolala kwenye makazi hayo.

Uongozi wa Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na  chenye Usajili wa NACTE kwa No. KOTETI/HAS/249 unatangaza nafasi ya masomo kwa muhula mpya wa SEPTEMBER-2022/2023 kwa kozi ya PHARMACY.