Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada ya kuingizwa kazini kwa Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Godfrey Tahona Walalaze, Mkurugenzi wa fedha na utawala CPA Peter John Singano pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs, leo tarehe 06/02/2022 katika Usharika wa Korogwe.Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki iliyoketi Utondolo Lushoto tarehe 9-10/12/2021 ilimthibitisha Mch. Godfrey Walalaze Kuwa Katibu Mkuu na CPA Peter John Singano kuwa Mkurugenzi wa fedha na Utawala.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 05/02/2022 ameongoza semina elekezi kuelekea siku ya kuingizwa kazini kwa Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze,Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, CPA Peter John Singano pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki hapo kesho tarehe 06/02/2022.
- Details

KKKT katika kutimiza wajibu wa kuwahudumia watu wake imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali tangu kuanzishwa kwake kupitia mipango mbalimbali,mojawapo ya mipango hiyo ni mpango wa 2015 - 2026 ambao umefanyiwa tathmini na kupata mpango mpya wa 2022- 2026.
- Details

Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mzee Joseph Jali ametoa wito kwa wana KKKT-DKMs,ndugu, jamaa na marafiki waliopo ndani na nje ya Dayosisi kuingia kazini ili kukamilisha ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Bangala Lutheran Junior Seminary ulio simama kwa takribuni miaka 20.
Page 89 of 124

