Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapa maagizo wakuu wa majimbo kusimamia shughuli nzima ya zoezi la kuhakikisha kila kijana anachangia bati moja katika ujenzi wa shule ya Bangala Lutheran Junior Seminary pia amewataka vijana watumie tamasha hilo kuunganisha mahusiano yao kwa kunyanyuana kiuchumi sambamba na kurudi kwa Mungu.
- Details

Mungu aliuumba ulimwengu mzuri na kutupa jukumu la kuutunza bila kujali dini yoyote kwani yakitokea madhara yanayo sababishwa na uharibifu wa mazingira huadhiri jamii nzima hayo yamesemwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 49 wa kujenga mahusiano mema kati ya Dini za Kiyahudi, Kikristo na Kiislamu( JCM), uliofunguliwa leo tarehe 22/02/2022 kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa SEKOMU.(JCM) ilianzishwa mnamo mwaka 1960, washiriki wakiwa ni Wakristo,Wayahudi na Waislam,lengo likiwa ni kuiasa jamii kutunza mazingira na kupambanua changamoto ya mabadiliko ya tabia ya Nchi.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza vijana wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kipekee vijana wa Kanisa Kuu Lushoto kwa kazi kubwa na nzuri waliyo ifanya kwa njia ya nyimbo na walio ongoza Ibada
pongezi hizo amezitoa leo tarehe 20/02/2022 kwenye Ibada ya sikukuu ya Vijana huku akimpongeza mratibu wa Vijana na ukwata wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Alice Kopwe kwa maandalizi mazuri yanayoondelea kuelekea tamasha la Vijana na Askofu litakalo fanyika tarehe 25-27/02/2022.
- Details

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Kalisti Lazaro ametoa wito kwa kamati ya amani ya viongozi wa Dini mbalimbali (Interfaith) kuendelea kuwa mabalozi wa kulinda amani na upendo kwa kuhubiri katika nyumba zao za Ibada ili kuzuia matukio ya ukatili pamoja na mauwaji ambayo yamekuwa yakishamiri maeneo mbalimba Nchini sambamba na kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa sensa ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu.
Page 88 of 124

