Nikasikia sauti  kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho wapate kupumzika baada ya taabuzao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nayo.

 

 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu   leo tarehe 21/01/2022 amekuwa na mwendelezo wa ziara ya kikazi katika Jimbo la tambarare na ameongoza kikao kazi kilichofanyika katika Usharika wa Korogwe, kikao hicho kilijumuisha Wachungaji, Mashemasi pamoja na wainjilisti wa KKKT-DKMs Jimbo la tambarare.

 

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu   leo tarehe 20/01/2022 amekuwa na ziara ya kikazi katika Jimbo la Kusini na ameongoza kikao kazi kilicho jumuisha Wachungaji, Mashemasi pamoja na wainjilisti wa KKKT-DKMs Jimbo la Kusini pamoja na mambo mengine yaliyo jadiliwa katika kikao hicho kilichofanyika katika Usharika wa soni Baba Askofu amewakumbusha watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa uwazi na umakini mkubwa katika kila jambo wanalo lifanya.

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 19/01/2022 ameongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji mstaafu Anthony Danga Mndeme katika Usharika wa Mamba jimbo la Kusini.