Mkuu wa Shirika la Michaeliskloster lililoko Hildesheim, Hannover nchini Ujerumani, Mch. Prof. Jochen Arnold ameitembelea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,ambapo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake na leo tarehe 15/06/2024 akiwa katika Chuo cha Biblia Vuga na kutoa zawadi ya Keyboard nzuri ili isaidie mafunzo ya kozi ya muziki inayotolewa Chuoni hapo.
Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amekutana na kufanya mazungumzo na Wanafunzi wa kozi ya Masters ya Kimataifa ya Usimamizi/Uongozi wa Diakonia ambao wameitembelea Dayosisi yetu kama sehemu yao ya mafunzo kwa njia ya vitendo.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amefanya Ziara ya kikazi nchini Philippines, kuanzia tarehe 15/5/2024 hadi tarehe 05/06/2024, Ziara hii iliyowezeshwa na chama Cha kiinjili Cha kimisioni, United Evangelical Mission (UEM) imekuwa na malengo ya kumuwezesha Baba Askofu kuhudhuria Makongamano mbalimbali ya Kimisioni katika Chuo Kikuu cha Silliman kilichopo katika Jiji la Dumaguete Mkoa wa Negros Oriental.

Ufunuo 14:13“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Madiga kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, anasikitika kutangaza kifo cha Bitrice David Mmbali kilichotokea  tarehe 27/05/2024 katika Hospitali ya Mloganzila iliyopo Jijini Dar Es Saalam alipokuwa anapatiwa matibabu.