Matukio katika Picha Ibada ya Mazishi ya Marehemu, Mchungaji Daniel Elierehema Kilangilo Magogo.Mchungaji Mstaafu Daniel Magogo aliitwa mbinguni tarehe 16/05/2024 na tarehe 20/05/2024 imefanyika Ibada ya mazishi yake Iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,Baba Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa. na mwili wa marehemu Mchungaji Mstaafu Magogo, umepumzishwa katika makaburi ya familia yaliyopo Kwesimu Lushoto.
  
KATIKA HISTORIA
KUZALIWA: - Marehemu Mch. Daniel Elierehema Kilangilo Magogo alizaliwa tarehe 16/09/1925. ELIMU YA MSINGI: - Alianza elimu ya msingi mwaka 1944 katika Shule ya Msingi Lushoto Extended Primary School. MIDDLE SCHOOL: - Alisoma Vugiri Middle School mwaka 1948 – 1951. KUBATIZWA: - Alibatizwa mwaka 1950 akiwa na miaka 25. ELIMU YA SEKONDARI: - Alisoma Tanga School mwaka 1952 hadi 1953.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akikabidhi vyeti kwa Vijana  11 wa KKKT-Dayosis ya Kaskazini Mashariki waliokuwa ziarani nchini ujerumani ambao pamoja na mambo mengine walifika nchini humo kwa ajili ya mafunzo ya  Water project titled water and Sanitation. Askofu Dkt. Mbilu, amegawa vyeti hivyo  katika Ibada ya Jumapili ya tarehe 12/05/2024 iliyofanyika katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Korogwe.

Kikao hiki kilifanyika kwa dhumuni la kumtambulisha Mkurugenzi wa Uchumi Mipango na Maendeleo Bibi. Pendo Lauwo kwa wakuu wa Idara pamoja na wakuu wa vituo vya uzalishaji. Baada ya utambulisho mkurugenzi alipata muda wa kueleza mikakati yake katika utekelezaji wa shughuli za kituo na wakuu wa Idara na vituo walitoa taarifa zao miezi mitatu. Kikao hiki kilifanyika  tarehe 15/06/2023 katika ukumbi wa mikutano Utondolo.