Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewataka Wakristo kuendelea kukemea vikali vitendo vya ukatili na viashiria vya mapenzi ya jinsia moja katika jamii kwani huo ndio msimamo wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, na Kanisa kwa ujumla.

Askofu Mch Dkt. Mbilu ametoa wito huo wakati akihubiri katika Ibada ya Jumapili ya  Pasaka iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto, ambapo amesema kuwa msimamo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Afrika kwa ujumla haliungi mkono ndoa wala mapenzi ya jinsia moja.

Sehemu ya salamu za Pasaka za Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu

Nawasalimu katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo!

 “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbiko lao waliolala” 1 Wakorintho 15:20.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amefungua rasmi Mkutano Mkuu  wa 4 baada ya Jubilee ya miaka 125 ya Injili KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, leo tarehe 30/03/2023 katika ukumbi wa mikutano  wa Benjamin William Mkapa Auditorium KOTETI Magamba.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amempongeza Mch. Happiness Diu kwa kuchaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa UEM Afrika kuwa mjumbe wa Bodi ya UEM kwa kanda ya Afrika nzima.