Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa Wainjilisti ni jeshi kubwa katika Dayosisi, linalofanya kazi kubwa na nzuri inayoonekana kwa kuwafikia wana Dayosisi kwa ukaribu zaidi.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 12/06/2022 kwenye Ibada ya Jumapili na kilele cha juma la Uinjilisti katika Dayosisi  ambapo  Wainjilisiti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wapatao 211 wameshiriki kwenye Ibada hiyo iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto.

Hata hivyo Askofu Dkt. Mbilu hakusita kuwajulisha Wainjilisti na Wanadayosisi  kwa ujumla juu ya ujio wa Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) ambacho kipombioni kukamilisha usajili wake ili kuanza udahili katika mwaka huu wa masomo wa 2022/2023.

 Ikumbukwe kuwa Askofu Dkt. Mbilu alipata wasaa wa takribani siku nne ya kukaa na  Wainjilisti  wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwenye semina iliyokuwa  na lengo la kuwajengea uwezo Wainjilisti hao hasa katika nyakati hizi zilizo jaa mafundisho potofu ya neno la Mungu semina hiyo  ilifanyika   katika ukumbi wa mikutano wa  Benjamin Mkapa SEKOMU ambapo pia Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu alipata nafasi ya kuwasikiliza Wainjilisti hao juu ya changamoto wanazo zipata na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi.

 

KATIKA PICHA: Semina ya Wainjilisti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Askofu iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa (SEKOMU) ambapo leo tarehe 11/06/2022 semina hiyo  imefungwa rasmi na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, hapo kesho Wainjilisti hao wanatazamiwa kushiriki Ibada ya Jumapili Kanisa Kuu Lushoto.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameahidi kusimamia Maslahi na kuboresha hali ya kiutumishi kwa kila Mwinjilisti aliyeajiriwa na Dayosisi ikiwemo kuwekewa michango katika mfuko wa hifadhi ya jamii na kwamba hakuna Mwinjilisti atakae staafu bila ofisi ya Askofu kujua.

Askofu Dkt. Mbilu ameeleza hayo leo tarehe 09/06/2022 wakati akifungua semina ya siku nne iliyoandaliwa kwa Wainjilisti  wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yenye lengo la kuwajengea uwezo,inayofanyika   katika ukumbi wa mikutano wa  Benjamin Mkapa SEKOMU.

 KATIKA PICHA: Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa awamu ya Tano KKKT-Dayosisi ya Konde Mch. Geoffrey S. Mwakihaba, Ibada hiyo imefanyika leo tarehe 05/06/2022, katika Usharika wa Kanisa Kuu tukuyu-Mbeya

na kuongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania (KKKT) Askofu Dkt.Fredrick Shoo huku Liturgia ikiongozwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

...............................

Hapo jana katika Ibada maalumu ya kuwekwa wakfu vifaa vya kiuaskofu iliyo ongozwa na Askofu Mstaafu wa Dayosisi hiyo  Askofu Dkt. Israel Peter Mwakyolile katika Usharika wa Kanisa Kuu tukuyu Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndiye aliye hubiri katika Ibada hiyo.