×

Warning

Failed deleting thumb_115_745.jpg

SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA PASAKA

JUMAPILI YA TAR. 15 MEI, 2022

NENO KUU:

"MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA" (KANTATE DOMINO)

"Kila mwenye pumzi na Amsifu Bwana"

ZAB.147:7--11

7 Mwimbieni Bwana kwa kushukuru, Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.8  Huzifunika mbingu kwa mawingu, Huitengenezea nchi mvua, Na kuyameesha majani milimani.9  Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.10  Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mtu.11  Bwana huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.

SIKU YA BWANA YA NNE INAYOFUATA PASAKA

 Mwimbieni Bwana wimbo mpya (Kantate Domino)

 AYA YA SIKU

"Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu" Zab.98:1

 SALA

Mwenyezi Mungu, wewe peke yako waweza kuzitawala nia za waaminio kwa umoja; Uwajalie watu wako kupenda uliyoyaamuru na kutaka uliyoyaahidi, ili katika dunia hii isiyo na raha, mioyo yetu istarehe huko kwenye furaha ya kweli. Kwa Yesu Kristo, Mwana wako na Bwana wetu. Amen.

SOMO LA 1: 2 The. 2:13--17

 13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;14aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.16 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, 17awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.

SOMO LA 2 MAHUBIRI:

Zab.104:33--35

33Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;34 Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia Bwana. 35 Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

KATIKA PICHA Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, akiwa Nchini Italy na Torre Pellice ambapo viongozi mbalimbali wa dini wamekutana na kuhudhuria kozi ya uongozi iliyokuwa inahusu maswala ya Uhamiaji na tamaduni katika jamii (migration and multicultural society) iliyo ratibiwa na Kanisa la Waldensian (Waldensian Church) Kanisa mwanachana wa UEM Nchini ujerumani (partner church of the UEM in Germany).

 

JUMAPILI ya Mei 9 mwaka 2021, shughuli za mji wa Lushoto na viunga vyake zilisimama kwa muda huku macho na masikio yote yakiwa kwenye tukio la Ibada ya kuingizwa kazini  kwa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kuwa Askofu wa awamu ya tano wa KKKT-DKMs.

Leo tarehe 09/05/2022 Askofu Dkt Msafiri Mbilu anafikisha mwaka mmoja tangu kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.Askofu Dkt  Mbilu anaendelea kuwakumbusha watumishi kusimama imara ili kuhubiri neno la Mungu kwa usahihi na kusimamia mafundisho sahihi ya neno la Mungu na kuondokana na mafundisho potofu yanayopelekea kujenga roho ya uvivu na wasiwasi katika jamii.

 Mhadhiri huyo mwandamizi wa chuo Kikuu cha Silliman cha Nchini Ufilipino, aliingizwa kazini katika Ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Lushoto na kisha yeye kumuingiza kazini Msaidizi wake, Mch. Michael Mlondakweli Kanju.

ILIVYOKUWA

Ibada ilianza kwa maandamano kutoka yalipo Makao Makuu ya Dayosisi hiyo, yaliyopo katikati ya Mji wa Lushoto na kuelekea Kanisa Kuu huku waki jipanga kwa kuongozwa na mbeba msalaba,

wabeba bendera ya Dayosisi na wapiga tarumbeta ambao walikuwa zaidi ya mia moja.Wapiga tarumbeta walikuwa kivutio kikubwa kwani walikuwa mahiri katika upigaji wao, pia walikuwa na sare ya pamoja ya mashati meupe na suruali nyeusi kwa wanaume na wanawake sketi nyeusi.

 

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kupitia kwa Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu umeanza utekelezaji wa ahadi waliyoitoa juu ya utaoji wa taarifa  ya  fedha zinazochangwa na Wanadayosisi zitakazo saidia kukabiliana na Deni la Dayosisi.

Ikumbukwe kua mnamo tarehe 24/03/2022 Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliwaandikia barua wana Dayosisi kuwaomba kuingia kazini ili kukabiliana na madeni makubwa yanayoikabili Dayosisi ambayo kwa ujumla wake ni hatarishi kwani yanaweza kusababisha mali za Dayosisi kupigwa mnada, kudumaza Dayosisi kwa muda mrefu, kutokuaminiwa na wadau wa maendeleo, kuathirika kwa Misioni pamoja na kufisha maono ya viongozi.