Uncategorised
- Details

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Leo tarehe 30/05/2022 imefanyika Ibada ya mazishi ya Marehemu Bibi,Hilgati A. Kika katika Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani. Marehemu Bibi,Hilgati Kika katika uhai wake alikuwa muimbaji wa kwaya Kuu KKKT-DKMs Usharika wa Makorora.

Marehemu Bibi,Hilgati ambaye pia ni mama mdogo wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, mwili wake umepumzishwa katika makaburi ya Bombo area Jijini Tanga.


Marehemu Bibi Hilgati alizaliwa tarehe 01/07/1948 katika Kijiji cha Kwang’wenda Wilayani Lushoto aliitwa mbinguni alfajiri ya tarehe 28/05/2022 katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga- Bombo.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu,Kwaya Kuu Makorora, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.


- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameendelea kuwa kumbusha Washarika wa Usharika wa Kange na Dayosisi kwa ujumla kuendela kuchangia Deni la Dayosisi na kusema kuwa taarifa ya michango hiyo itaendelea kutolewa kama ilivyo fanyika awali.

amewakumbusha Washarika hao leo tarehe 29/05/2022 ni siku ya Bwana kabla ya Pentekoste, SIKU YA CCT Neno Kuu (Sikia Kuomba kwetu) Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kange na kuwasihi Washarika na Wanadayosisi kuona umuhimu wa kutoa sadaka ya CCT.
- Details

KATIKA PICHA Ibada ya ndoa kati ya Mtheologia Jonathan Denisi Hiza na Bi. Neema Simoni Mbilu. iliyofanyika leo tarehe 28/05/2022 katika Usharika wa Pongwe Jimbo la Pwani. Ndoa hiyo imefungwa na Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Mlondakweli Kanju akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus Ketto.
- Details

Page 81 of 124

