Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye ambatana na Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Michael M. Kanju,Kaimu Katibu Mkuu Mch.Godfrey T. Walalaze,ndugu David Chanyenghea ambae ni Kaimu mkurugenzi wa Uchumi na Mipango  wamepata nafasi ya kushiriki katika ibada  ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la  KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Arusha mjini-Kanisa Kuu leo tarehe 11 Aprili, 2021 .

Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 10 Aprili, 2021 amekutana na wana Dayosisi  wazawa kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, marafiki na wadau mbalimbali  wanaoishi katika Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine ya jirani na kufanya kikao  katika ukumbi wa Umoja Hostel Mkoani humo ambapo amepata nafasi yakuelezea hali ya Dayosisi ilivyo, huku kukishuhudiwa muamko mkubwa kutoka kwa wana Dayosisi hao.Ambapo wamepata nafasi ya kuchangia na kushauri mambo mbalimbali yatakayo leta mafanikio katika Dayosisi.

Askofu Mteule Mch.Dkt.Mbilu amewashukuru kwa kuonesha moyo na nia thabiti ya kushirikiana na washarika pamoja na marafiki  wengine kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na wadau.
Ameongeza  kuwa lengo la kukutana ni kupata nafasi ya kuelezea juu ya hali ya Dayosisi na kuahidi uwazi katika uendeshaji wa Dayosisi na kuhakikisha ripoti za vyanzo  vyote vya mapato vinawafikia washarika kila baada ya miezi mitatu.



Kilele cha harambee hiyo kwa awamu ya kwanza kitafanyika tarehe 25 Aprili,2021 katika usharika wa Korogwe jimbo la Tambarare kwa  lengo la kukusanya Tsh. Bilioni mbili (2,000,000,000.)

Mch. Dkt. Msafiri Mbilu  ameambatana na Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Michael Kanju,Kaimu Katibu Mkuu Mch.Godfrey T. Walalaze pamoja na ndugu David Chanyenghea ambae ni Kaimu mkurugenzi wa Uchumi na Mipango.

 

Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema (Mt. 28:5-6).

Wapendwa katika Bwana, kufufuka kwa Yesu ni tukio la imani kubwa kwetu sote tunaoamini juu ya nguvu ya ufufuo. Tukio hili linaondoa hofu inayotanda mioyoni mwa wengi juu ya kifo na nguvu ya mauti.

Tunasherehekea Pasaka wakati ambapo mioyo ya wengi imejawa na hofu kubwa ya magonjwa ya kutisha yanayosikika mahali pote duniani, misiba ya kutisha ya kuondokewa na wapendwa wetu. Haya yote yanatuletea mahangaiko na majonzi.

Katikati ya haya yote tunapokea ujumbe mkubwa wa matumaini Malaika anaposema “msiogope”.Tangazo hili la Malaika la kutuondolea hofu linaleta tumaini kubwa kwamba yupo mtangulizi ambaye ameshinda kifo na nguvu ya mauti. Yesu mfufuka analeta tumaini la kutokuogopa kifo na nguvu ya mauti kwetu tunaoamini. Kufufuka kwake hakujatokea kwa bahati mbaya bali ni mpango kamili wa Mungu katika historia ya ukombozi wetu sisi wanadamu. Hii ndiyo maana malaika anakiri akisema “amefufuka kama alivyosema”.

Tuitegemee nguvu ya Mungu iliyomfufua Yesu kuwa sasa tunaye mshindi aliyetutangulia na kwamba sisi sote tunaomwamini hatuna sababu ya hofu ya mauti kwani Bwana amefufuka kutoka kwa wafu.

Huyu Yesu aliyefufuka akaendelee kutujaza matumaini mapya, kwetu mmoja mmoja, matumaini katika familia zetu na jamii kwa ujumla.

 

....................................................................................