Mwl. Christopher Mwakasege asubuhi ya leo tarehe 11/02/2021 amepata nafasi ya kutembelea Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo pia ameshiriki katika Sala ya asubuhi.

 

Msaidizi wa  Askofu ,Mch. Michael Kanju ambaye aliambatana na Mratibu wa Misioni na Uinjilisti Mch John Ndimbo. wamepata nafasi ya kumpokea Mwl. Christopher Mwakasege ambaye hapo kesho atapata nafasi ya kushiriki na kufundisha Neno la Mungu katika Mkutano wa wachungaji ulioanza leo tarehe 10/02/2021

uliofunguliwa na Mhe. Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Mbilu katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.

Ikumbukwe Mwl. Christopher Mwakasege atapata nafasi ya kufundisha neno la Mungu katika semina itakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 12/02/2021 Kanisa Kuu Lushoto Cathedral.

 

 

 

Kaimu katibu Mkuu Mch. Godfrey T. Walalaze leo tarehe 05/02/2021 amehitimisha Semina elekezi ya mafunzo ya kuimarisha Vituo vya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki iliyo anza jana Katika ukumbi wa mikutano Cathedral ambapo amegusia mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuzijua Kanuni, Sheria na Taratibu za Kazi.