Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,Watanzania wote pamoja na ndugu waliopoteza wapendwa wao, kufuatia maafa ya mafuriko, yaliyosababishwa na mmomonyoko wa ardhi kufuatia kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang uliopo Mkoani Manyara ambao ulikuwa na miamba dhoofu iliyonyonya maji na kusababisha maporomoko na hivyo kutengeneza tope ambapo pamoja na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha tope hilo lilisambaa katika makazi ya watu na kusababisha maafa makubwa.
Askofu Dkt. Mbilu ametoa salamu hizo tarehe 10/12/2023 kwenye Ibada ya Jumapili ambayo inafunga kalenda ya matukio ya Dayosisi iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto na kusisitiza kuwa Kanisa linaungana na Wananchi waliokumbwa na maafa hayo ya mafuriko na hivyo kuagiza Jumapili ya Tarehe 17/12/2023 kuwepo na maombi maalumu yatakayo ambatana na toleo maalumu (SADAKA) itakayo tolewa katika Sharika zote za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, na ili kiasi cha pesa zitakazo patikani zitakabithiwa kwa uongozi wa Serikali kama sehemu ya Mkono wa pole kufuatia maafa hayo.
MBUNGE WA LUSHOTO MHE. SHABANI SHEKILINDI
Naye Mbunge wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Shekilindi ameunga mkono jitihada za Askofu Dkt. Mbilu katika kuhakikisha deni lote la Dayosisi linamalizika kwa kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili na Elfu Kumi(1,210,000/=) na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Kanisa.
Ibada hii ilihudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Dayosisi akiwemo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Bi. Ikupa Harsoni Mwasyoge, ambaye katika salamu zake ameishukuru KKKT-DKMs, kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira.
Hata hivyo Mhe. Ikupa Mwasyogenaye, amemshukuru kipekee, Askofu Dkt. Mbilu kwa kuagiza sharika za KKKT-DKMs, kufanya changizo maalumu la kutoa sadaka na vitu mbalimbali Jumapili ya tarehe 17/12/2023 kwaajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko Mkoani Manyara kwani kwa kufanya hivyo ni sehemu ya kuunga mkono wito alioutoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya kuwasaidia waathirika hao.
DEAN MICHAEL MLONDAKWELI KANJU
Katika Ibada hii jumla ya vijana 71 walibarikiwa na wa 5 kubatizwa ambapo kwenye risala yao waliyoisoma kwa Baba Askofu Dkt. Mbilu, wamesema kuwa wanatambua kazi kubwa inayofanywa na KKKT-DKMs katika kumhudumia mwanadamu kiroho, kimwili na kiakili na hasa kazi za maendeleo zinazoendelea kufanyika, huku wakiahidi kwenda kuwa vijana wenye nidhamu na watii katika Kanisa na jamii kwa ujumla.
Vijana wa kipaimara walitoa kiasi cha Tsh 250,000 kwaajili ya kuchangia ulipaji wa deni la Dayosisi, ambapo pia waliomba kuungwa mkono na wazazi,walezi pamoja na washarika walioshiriki katika Ibada na kufanikiwa kukusanya jumla ya Ths. 3,448,550/= ambapo fedha hizo zimeelekezwa katika kulipa deni la Dayosisi.
MKUU WA JIMBO LA KUSINI. MCH. ISSAI AMASIA MWETA