Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amekutana na kufanya mazungumzo na Wanafunzi wa kozi ya Masters ya Kimataifa ya Usimamizi/Uongozi wa Diakonia ambao wameitembelea Dayosisi yetu kama sehemu yao ya mafunzo kwa njia ya vitendo.
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara yao katika Dayosisi yetu tayari wamepata nafasi ya kutembelea vituo vyetu vya kidiakonia ili kuona namna shughuli za kidiakonia zinavyofanyika.
Vituo walivyovitembelea ni pamoja na Irente Chidren's Home, Irente School for the blind, Irente Rainball School, Bumbuli Hospital, Emao Compassion program na Lutindi Mental Hospitali.
Aidha wametembelea Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto na Usharika wa Korogwe ili kuona namna Diakonia inavyofanyika katika ngazi ya sharika. Idadi ya wanafunzi hao ni 14 wakiwa wameongozana na viongozi wao wawili kutoka Chuo Kikuu cha Bielefeld na UEM nchini Ujerumani. Baba Askofu Dkt. Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo hayo na wanafunzi hao leo tarehe 14/06/2024-Makao Makuu ya Dayosisi Lushoto Tanga.