Mkuu wa Shirika la Michaeliskloster lililoko Hildesheim, Hannover nchini Ujerumani, Mch. Prof. Jochen Arnold ameitembelea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,ambapo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake na leo tarehe 15/06/2024 akiwa katika Chuo cha Biblia Vuga na kutoa zawadi ya Keyboard nzuri ili isaidie mafunzo ya kozi ya muziki inayotolewa Chuoni hapo.
Awali mgeni huyu alipatana nafasi ya kutembelea Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yaliyopo Lushoto Tanga na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.
Shirika hilo ambalo pia lina Chuo cha Mafunzo ya Muziki kwa muda mrefu sasa kimekuwa na uhusiano na Chuo cha Biblia Vuga kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki .