HABARI KWA UFUPI: Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,amesema kuwa mipango ya uanzishwaji wa kozi ya muziki katika Taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) inaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na vifaa vitakavyo tumika katika kufundishia kuanza kupatikana.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 22/01/2025 akiwa katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yaliyopo Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga, mara baada ya kupokea ugeni wa marafiki kutoka Bethel Ujerumani.

Ugeni huu unaongozwa na Bw.Werner Jakob Blauth, ambaye alishaawahi kufanya kazi katika kituo cha Lutindi Mental Hospital kinachomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Aidha Askofu Dkt. Mbilu, ameongeza kuwa ugeni huo umetembelea KKKT-Dayosisi Kaskazini Mashariki kwa lengo la kuona baadhi ya vituo vya Diakonia vya Dayosisi ikiwemo kituo cha Irente children's Home, Irente Rainbow School, Irente School for the Blind pamoja na Hospital ya wagonjwa wa akili (Lutindi Mental Hospital) ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika vituo hivyo.

Vifaa vilivyo pokelewa leo ni pamoja na Tarumbeta filimbi vikiwa ni alama tu ya vifaa vingine vingi vya muziki ambavyo vipo nchini Ujerumani vikiwa katika hatua za mwisho kusafirishwa kuja katika Dayosisi yetu.

Hata hivyo Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, amewashukuru wageni hao kwa mchango wao mkubwa wa kutoa vifaa hivyo vya muziki ikiwa ni ishara ya kuendelea kuonyesha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Dayosisi na marafiki hao kutoka Ujerumani.