Leo tarehe 16 Oktoba 2021 kumefanyika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Lwandai inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ambapo wanafunzi 41 (wavulana 23 na wasichana 18 ) wamehitimu. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni Mhasham Askofu, Dkt Msafiri Joseph Mbilu aliyewakilishwa na Msaidizi wa Askofu , Mchungaji Michael Mlondakweli Kanju. Mahafali hayo yalifana sana yakipambwa na vishirikisho mbalimbali toka kwa wahitimu na wanafunzi wengine.

Kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, 1922-1999 (Nyerere Day)

 

Leo tarehe 10/10/2021 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada  ya sikukuu ya mavuno, katika  Jimbo la Pwani, Usharika wa Kana.

Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.