ELCT North Eastern Diocese
Askofu Mstaafu Joseph Jali awashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Details
Nyumba hubarikiwa ukaamo,Yesu,uliye mpenzi wa moyo,wakukaribishapo kwa furaha,uliye mgeni wa heshima kuu.mioyo yetu inapokupenda na macho Yote yakungojapo, midomo yote ikuulizapo, na watu wote wanapokutii.
- Hits: 7760
Ibada ya Kipaimara Kanisa Kuu Lushoto
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 12/12/2021 ameongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika wa Kanisa Kuu (Cathedral) Lushoto,ambapo jumla ya vijana 86 wamebarikiwa na watano kati yao walibatizwa.
Kulingana na kalenda ya matukio ya Dayosisi Baba Askofu Dkt. Mbilu anahitimisha matukio haya huku jumla ya vijana walio barikiwa ikiwa ni 1888 na Wakristo watu wazima waliobazitwa kwa mwaka huu ni 286.
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akimbatiza mmoja wa vijana walio batizwa
Baba Askofu amewashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa matendo hayo Mkuu yaliyo tendeka katika kipindi hiki.Baba Askofu ameendelea kusisitiza yeye akiwa mmoja wa wadhamini wa mali za Dayosisi atahakikisha kwa kushirikiana na viongozi wengine mali za Dayosisi hazichezewi na zinabaki kuwa salama.
Kwa upande mwingine Askofu Dkt. Msafiri Joseph mbilu kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki amemtambulisha Mch. Godfrey Tahona Walalaze kuwa sasa ndiye Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki. Hii nikutokana na kuthibitishwa na Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki aliyo keti hivi kalibuni.Mwingine aliye thibitishwa na Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ni CPA Peter Singano ambaye sasa rasmi ndiye Mkurugenzi wa Fedha na utawala KKKT-DKMs
Mch. Michael Mlondakweli Kanju,Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs (Kushoto), Mch. Godfrey Tahona Walalaze ,Katibu Mkuu KKKT-DKMs,katika picha na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.
Katika Risala ya vijana waliobarikiwa kipekee wamemshukuru Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki.Mzee Mathayo Joseph Jali kwa moyo wake na kuona kwamba Watoto wake, wajukuu na vitukuu vyake vinapata elimu,ameonesha juhudi hizo kutokana na maadhimisho ya miaka 60 ya ndoa yake na Bibi Sara Jali kwamba kipaumbele cha maadhimisho hayo ameamua kuweka alama katika Shule ya BANGALA Lutheran Junior Seminary inayo milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki.
Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki.Mzee Mathayo Joseph Jali pamoja na Bibi Sara Jali
Vijana hao wamewashukuru walimu wao waliowafundisha mafundisho sahihi ya neno la Mungu katika kipindi chote cha miaka miwili,Mch . Edward Msocha,PW Eveline Shekindo , Mwj. Naftari Siafu na Ester Mahimbo.Darasa hilo pia lilikabidhiwa kwa Mch. Anderson Kipande,hadi leo vijana hao wanapo barikiwa darasa hilo limekuwa chini ya Mch.Emmanuel Mweta na Mch. Charles Lumwe.
Mafundisho hayo sahihi waliyo yapata vijana hao yamepelekea kukiri mbele ya Baba Askofu kuwa watakuwa vijana wenye nidhamu, watiifu sasa wanapo ingia katika rika la watu wazima baada ya kubarikiwa kwao na kuongezwa kuwa kamwe hawata yumbishwa na mafundisho potofu ya Neno la Mungu yaliyo ikumbu Dunia katika kipindi hiki.
- Hits: 8480
Taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Dayosisi yakabidhiwa Mbele ya Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs
- Details
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akipokea taarifa ya Tume Maalum ya kupitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Dayosisi kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume hiyo W.S Msagati, taarifa hiyo imekabidhiwa mbele ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe 10/12/2021.
- Hits: 7481
Tanzia-Baba mzazi wa Askofu , Dkt. Alex Gehaz Malasusa amefariki
- Details
- Hits: 8799
Page 66 of 108